0

Presha ya homa ya pambano la Yanga na Simba
imezidi kupanda kila upande ukijitapa kuibuka na
ushindi katika mchezo huo wa J'mosi
YANGA: NUKUU ZA HANS VAN DER PLUIJM NA
NADIR "CANNAVARO" HAROUB
Kocha Hans Pluijm wa Yanga amesema mchezo
huo hauwapi presha kwenye kambi yao kwani
Simba ni timu ya kawaida kama ilivyo timu
nyingine na ndiyo maana wamekuwa wakifanya
mazoezi mepesi ili kujiandaa kuchukua pointi zao
tatu kama ilivyokuwa msimu uliopita.
Pluijm ameiambia Goal , pamoja na kusajili
wachezaji wengi wapya lakini hajaona mabadiliko
ya wapinzani wao licha ya kushinda mechi tano
za ligi ya Vodacom na hilo watalidhihirisha
Jumamosi watakapokutana uwanja wa taifa.
“Nikweli tumepoteza mchezo mmoja dhidi ya
Stand lakini hainamaanishi kwamba na Simba
watatufunga inawezakana Stand waka bora kuliko
Simba, ndiyo maana kama kocha nimekuwa
nikitoa maelekezo ya kawaida kwa wachezaji
wangu kwasababu naamini tutashinda,”amesema
Pluijm
Mdachi huyo amesema msimu uliopita alivuna
pointi sita na mabao manne kutoka kwa Simba
msimu huu anataka kutengeneza rekodi nyingine
kwa kuchukua pointi sita na mabao 10 katika
mechi zote mbili.
Kwaupande wake nahodha wa Yanga Nadiri
Haroub ‘Cannavaro’ amewataka mashabiki wa
timu hiyo kuondoa hofu na kufika kwa wingi
uwanjani Jumamosi ili kushuhudia wakiifunga
Simba kipigo cha aibu.
Cannavaro ameiambia Goal , anajua timu
wanayokutana nayo imejidhatiti lakini mapungufu
waliyokuwa nayo hayawezi kuwapa ushindi mbele
ya kikosi chao bora ambacho kinarekodi nzuri
dhidi ya timu inayokutana nayo Simba
“Nawaomba mashabiki wetu waje kwa wingi ni
mchezo mzuri na wenye ushindani lakini baada
ya dakika 90 Yanga ndiyo atakuwa mshindi kama
ilivyokuwa msimu uliopita na hilo linatokana na
ubora wa kikosi chake licha ya kwamba
tumeoteza mchezo wao hawajapoteza,”amesema
Cannavaro.


SIMBA: NUKUU ZA JOSEPH OMOG NA JONAS
MKUDE
Naye kocha wa Simba Joseph Omog, amesema
nimchezo mgumu kwasababu unazikutanisha
timu zenye upinzani mkubwa lakini anaamini
timu yake itapata ushindi kutokana na kasi
waliyoanza nayo msimu huu.
Omog raia wa Cameroon ameiambia Goal , ushindi
walioupata dhidi ya Azam umempa matumaini ya
kubaini kuwa timu yake inaweza kupata matokeo
mbele ya timu kubwa kama Yanga na hilo ndilo
linampa matumaini ya kushinda mchezo huo.
“Ninazitaka pointi tatu za Yanga najua haitakuwa
kazi rahisi kutokana na uimara wa wapinzani
wetu lakini nimekiandaa kikosi changu kwa ajili
ya kupambana kwa dakika zote na kupata
matokeo zaidi tutaona baada ya dakika 90,”
amesema Omog.
Kwaupande wake nahodha wa Simba Jonas
Mkude amesema wamejipanga kufuta uteja kwa
kuifunga Yanga Jumamosi kutokana na
maandalizi waliyofanya na kasi waliyokuwa nayo
hivi sasa.
Mkude ameiambia Goal ,kwa kikosi walichokuwa
nacho msimu huu haoni sababu ya kushindwa
kuifunga Yanga kwasababu wao ndiyo timu bora
kwa sasa tofauti na ilivyokuwa kwa wapinzani
wao na ndiyo maana wanaongoza ligi huku
wakiwa hawajapoteza hata mchezo mmoja.
“Simba ndiyo bingwa msimu huu na Jumamosi
ndiyo tutathibitisha haya ninachoweza kusema
nimchezo wenye ushindani lakini uhakika wa
ushindi ni mkubwa kutokana na ubora tuliokuwa
nao sisi Simba msimu huu,”amesema Mkude
Huo nimchezo wa kisasi kwasababu Simba
iliyopoteza mechi zote mbili msimu uliopita
haitakubali tena matokeo kama yale na ndiyo
maana imefanya usajili mzuri wa kusajili
wachezaji wapya 11, ili kurudi kwenye ushindani
kama ilivyokuwa kwa wapinzani wao Yanga.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top