Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya
Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa
ametaja majina ya nyota 24 watakaounda kikosi
ambacho kitasafiri mwishoni mwa wiki ijayo
kwenda Addis Ababa, Ethiopia kucheza na wenyeji
wetu kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa
utakaofanyika Oktoba 8, mwaka huu.
Mkwasa maarufu kwa jina la Master amesema
wachezaji aliowaita wataingia kambini Oktoba 2,
2016 kabla ya kuanza kukiandaa kuanzia Oktoba 3,
2016 ikiwa mara baada ya michezo ya Ligi Kuu
Tanzania Bara ya mwishoni mwa wiki hii ambako
Mwadui itacheza na Azam huku Mbao ikishindina
na JKT Ruvu Oktoba 2, mwaka huu.
Nyota wa Stars walioitwa na Mkwasa ni:
Makipa
Deogratius Munishi – Young Africans
Said Kipao – JKT Ruvu
Aishi Manula – Azam FC
Mabeki
Shomari Kapombe – Azam FC
Juma Abdul – Young Africans
Vicent Andrew - Young Africans
Mwinyi Haji - Young Africans
Mohamed Hussein – Simba SC
David Mwantika - Azam FC
James Josephat – Tanzania Prisons
Viungo wa Kati
Himid Mao - Azam FC
Mohammed Ibrahim – Simba SC
Jonas Mkude – Simba SC
Muzamiru Yassin – Simba SC
Viungo wa Pembeni
Shiza Kichuya – Simba SC
Simon Msuva - Young Africans
Juma Mahadhi - Young Africans
Jamal Mnyate – Simba
Hassan Kabunda – Mwadui FC
Washambuliaji
Ibrahim Ajib – Simba SC
John Bocco - Azam FC
Mbwana Samatta - CK Genk ya Ubelgiji
Elius Maguli – Oman
Thomas Ulimwengu – TP Mazembe Congo
Mchezo huo utakaofanyika jijini Addis Ababa,
umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa
na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa
wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao.
Shirikisho la Mpira wa Miguu la Ethiopia (EFF),
wameo
Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo
huo kwa maana kina alama za nyongeza kama
inatokea unaifunga timu mwenyeji.
Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu
kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za
taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 132
kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa
ubora. Ethiopia yenyewe inashika nafasi ya 126.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji
anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa
wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C
Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu
nyingine bora kimataifa ni Ujerumani, Colombia na
Brazil.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 34
kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na
Algeria, Senegal, Tunisia na Ghana.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.