0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania
anayekipiga katika klabu ya KRC Genk ya ligi kuu
ya Belgium – Jupiter League – Mbwana Ally
Samatta, jana kupitia akaunti ya Instagram
ameonyesha ‘ndinga’ yake aliyoinunua baada ya
kupata leseni ya kuendesha gari nchini Belgium.
Samatta ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa wiki
kadhaa baada ya kupata majeruhi, jana usiku
alikuwemo katika katika kikosi cha Genk
kilichoifunga Sassuolo 3-1 katika mchezo wa
Europa League.
Gari alionunua Samatta ni Merecedez Benz Cla220
Cdi AMG Sport 2016 – ambayo imemgharimu kiasi
cha €46,680 ambayo ukiizidisha kwa fedha za
madafu inakuwa zadi ya millioni 130.
Inakadiriwa Mbwana Samatta ambaye ana mkataba
na KRC Genk mpaka 2020, analipwa kiasi cha dola
35,600 kabla ya kodi kwa mwezi.




ShaffihDauda



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top