Joseph Omog ameendelea kuilinda rekodi yake
ya kutopoteza mechi msimu huu baada ya sare
dhidi ya Yanga.
Yanga na Simba zimegawana pointi kufuatia sare
ya goli moja kwa moja kwenye mchezo wa Ligi
Kuu Tanzania Bara.
Yanga ndio walikuwa wa kwanza kupata goli
kupitia Mrundi Amis Tambwe kufuatia pande zuri
kutoka kwa Mbuyu Twite wakati dakika zikielekea
ukingoni Wekundu wa Msimbazi walisawazisha
kupitia kwa winga wao Shiza Kichuya.
Mchezo huo ulitawaliwa na vurugu na kupelekea
kapteni wa Simba Jonas Mkude kupata kadi
nyekundu kwa kumsukuma mwamuzi wa
mchezo.
1.Muda umefika Joseph Omog kumuamini Juuko
Murshid
Murshid alionesha ukomavu kwenye eneo la
ulinzi kwenye mechi dhidi ya Yanga kwa muda
mchache aliocheza , aliingia kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Novatus Lufungo ambaye
alionesha mechi kumshinda na kupelekea
kucheza rafu mara kwa mara , bila mwalimu
kumtoa mapema huenda naye angemaliza
mchezo kwa kadi nyekundu benchi la ufundi
Wekundu wa Msimbazi ni wakati wa kutengeneza
umoja wa Mwanjale na Muurshid.
2). Shiza Kichuya ndiye mchezaji hatari kwenye
kikosi cha Simba
Ukitaka kuizuia Simba kwa sasa hakikisha
Kichuya hapati nafasi ya kutawala, amefunga
magoli matano kwenye michezo saba mpaka
sasa, ndiye kinara wa upachikaji magoli Ligi Kuu
Bara, kwenye mchezo dhidi Yanga Kichuya
alionesha ubora wa hali ya juu licha ya kucheza
pungufu kwa sasa.
3) Tatizo la marefa bado changamoto kwenye
mpira wetu
Kila mwaka matatizo ya waamuzi yamekuwa
changamoto hapa nchini, tangu mwanzo wa
mchezo Martin Sanya alionekana kushindwa
kuendana na kasi ya mchezo, alishindwa kutafsiri
sheria vizuri kwa baadhi ya maamuzi na
kupelekea mchezo kuwa na vurugu ndani yake.
4) Uchovu unaigharimu Yanga kwa sasa
Licha ya Simba kucheza pungufu kwa takribani
dakika sabini ya mchezo ila Wana Jangwani
walishindwa kuondoka na alama tatu, uchovu wa
kutopumzika kwa wachezaji tangu msimu uliopita
umeonekana kwenye mechi na Simba, timu
nzima ilicheza vibaya hasa kipindi cha pili na
kuonekana wamekata upepo hivyo kuwaruhusu
Simba kurudi mchezoni na kupelekea
kusawazisha dakika za lala salama.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.