0

Aliyekuwa Meneja wa timu ya Taifa ya Uingereza,
Sam Allardyce anaweza kufungiwa na chama cha
soka nchini humo, FA baada ya uchunguzi wa
sakata lake kukamilika.
Allardyce anadaiwa kuahidi kutoa maelekezo ya
udanganyifu katika usajili wa wachezaji. Waandishi
wa Gazeti la Daily Telegraph ndio waliomuweka
mtegoni baada ya kujifanya wafanyabishara na
yeye kuahidi kuwaelekeza nini cha kufanya
kuwezesha udanganyifu huo.
FA imesema inasubiri ripoti kamili ya Daily
Telegraph ili kubaini kama mkufunzi huyo wa
zamani wa Sunderland atatozwa faini au kufungiwa
kabisa.
Allardyce alikuwa kujiuzulu Septemba 27 kufuatia
sakata hili.Ametumikia nafasi yake kwa siku 67 tu.
Gareth SouthGate aliyekuwa msaidizi wake
aliteuliwa kuwa kocha wa muda 'Caretaker
Manager'.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top