Jana Ijumaa usiku kulikuwa na mchezo mmoja wa
ligi kuu ya Uingereza ambapo Everton ilikuwa
mwenyeji wa Crystal Palace katika mchezo
uliopigwa kwenye dimba la Goodison Park.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1,
Romelu Lukaku, mchezaji wa Kimataifa wa Ubelgiji
akiwa wa kwanza kuifungia Everton bao ambalo
lilisawazishwa na Christen Benteke mshambuliaji
mwingine wa timu ya Taifa ya Ubelgiji.
Lukaku alifunga kupitia mpira wa adhabu alioupiga
akiwa umbali wa takribani mita 20 wakati lile la
Crystal Palace Benteke alilifunga kwa kichwa
akiunganisha krosi ya Joel Ward.
Palace wangeweza kuondoka na ushindi kama bao
la Damien Delaney lisingekataliwa na mwamuzi.
Damien Delaney alifunga bao hilo ambalo
lilikataliwa na mshika kibendera kwa kuwa
mfungaji alikuwa ameotea.
Everton imepanda hadi nafasi ya tatu katika msimu
wa EPL ikiwa na pointi 14, Palace iko nafasi ya
saba baada ya kufikisha pointi 11.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.