0

Klabu ya soka ya Liverpool jioni hii
imetoka nyuma kwa goli 1 na kupachika
goli 2 na kuchomoka na ushindi wa
mabao 2 kwa 1 dimbani Libert
walipokwaana na Swansea City kwenye
Ligi Kuu!
Meneja hatarini!
Meneja wa Swansea City aitwaye
Francesco Guidolin yupo kwenye hati
hati ya kutimuliwa!
Goliii!
Hii ni kutokana na mwendo mbovu wa
klabu yake. Kwenye mechi hiyo walianza
kupachika goli kwa goli la Leroy Fer
mnamo dakika ya 8 ya mchezo huo.
Kipindi cha pili, Firmino alirejesha goli
dakika ya 54 na goli la pili likafungwa na
James Milner kwa penati dakika ya 84
ya mchezo ule.
Msimamo
Sasa kwa ushindi huu klabu ya soka ya
Liverpool inakwea mpaka nafasi ya pili
wakiwa na alama 2 nyuma ya vinara
Manchester City waliokipiga mechi 1
pungufu kwenye ligi hii.
Refa na vikosi
Refa alikuwa ni Michael Oliver. Swansea
walikuwa na Fabianski; Rangel, van der
Hoorn, Amat, Naughton; Fer, Cork,
Britton; Routledge, Borja na Sigurdsson.
Akiba: Nordfeldt, Mawson, Taylor, Fulton,
Ki, Barrow na McBurnie.
Kwa upande wao Liverpool walikuwa na
Karius; Clyne, Lovren, Matip, Milner;
Lallana, Henderson, Wijnaldum; Mane,
Firmino na Coutinho. Akiba: Mignolet,
Sturridge, Klavan, Moreno, Lucas, Can na
Origi.



Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top