WATANI wa jadi, Simba na
Yanga wamegawana pointi
baada ya kutoa sare ya
kufungana bao 1-1 katika
mchezo wa Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara jioni
ya leo Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Ushindi unazidi kupandisha
kileleni Simba SC ikifikisha
pointi 17, baada ya kucheza
mechi saba, wakati Yanga
inatimiza pointi 11 baada ya
kucheza mechi sita.
Katika mchezo wa leo Yanga
walitangulia kwa bao la
Mrundi, Amissi Joselyn
Tambwe kabla ya mzalendo,
Shizza Ramadhani Kichuya
kuisawazishia Simba SC
iliyocheza pungufu kwa
muda mrefu baada ya Jonas
Mkude kutolewa kwa kadi
nyekundu kipindi cha
kwanza.
Tambwe alifunga bao lake
dakika ya 26, akimalizia pasi
ndefu ya beki Mbuyu Twite
na kugeuka mbele ya beki
wa Simba, Novat Lufunga
kabla ya kufumua shuti
lililomshinda kipa Vincent
Angban.
Bao hilo lilizua kizaazaa,
wachezaji wa Simba
wakimvaa refa Martin Saanya
wakidai mfungaji, Tambwe
aliushika mpira kabla ya
kufunga.
Katika vurugu hizo, Saanya
akamtoa kwa kadi nyekundu
Nahodha wa Simba SC,
Jonas Mkude dakika ya 29
kwa sababu ndiye aliyekuwa
mstari wa mbele.
Na mchezo ukasimama kwa
takriban dakika tano baada
ya mashabiki wa Simba
kuanza kufanya vurugu
waking’oa viti na kutupa
uwanjani.
Polisi walitumia milipuko
kuwatuliza mashabiki hao na
mchezo ukaendelea.
Kipindi cha pili, Simba SC
walibadlika pamoja na
kucheza nguvu wakafanikiwa
kupata bao la kusawazisha
lililofungwa na winga Shizza
Kichuyaa dakika ya 87 baada
ya kona aliyochonga kuingia
moja kwa moja nyavuni.
Kikosi cha Yanga SC
kilikuwa; Ally Mustafa
'Barthez',Juma Abdul,Mwinyi
Hajji, Kevin Yondan/Andrew
Vincent dk46, Vincent
Bossou, Mbuyu Twite, Juma
Mahadhi/Simon Msuva,
Thabani Kamusoko, Amisi
Tambwe, Donald Ngoma na
Deus Kaseke/Haruna
Niyonzima.
Simba SC; Vincent Angban,
Janvier Besala Bokungu,
Mohammed Hussein
'Tshabalala', Novart Lufunga/
Juuko, Method Mwanjali,
Jonas Mkude, Shizza
Kichuya, Muzamil Yassim,
Laudit Mavugo/Blagnon,
Ibrahim Hajib/Mohamed ‘Mo’
Ibrahim na Mwinyi Kazimoto.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.