0


Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 Serengeti Boys imeshindwa kufuzu kucheza
fainali za vijana Barani Afrika kwa kutupwa nje na
Congo Brazaville.

Africa Newss Sports tumepata matokeo toka uwanjani yanayothibitisha kwamba Serengeti Boys imeshindwa kufuzu baada ya kukubali
kufungwa goli pekee katika mchezo wa leo dhidi ya
Wenyeji ikiwa ni goli la dakika ya 92 wakati wengi
wetu tukiamini kwamba vijana hao wamefuzu kama
mchezo ungemalizika kwa sare ya bila kufungana.

Matokeo ya bao 3-2 ambayo Serengeti iliyapata wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam ndiyo yamewaangusha leo kwani Congo Brazaville
wamenufaika na faida ya goli la ugenini huku Serengeti boys ikishindwa kufunga bao lolote
ugenini.

Mioyo ya Watanzania Wapenda Soka waliweka matumaini makubwa kwa timu hii kutokana na kiwango bora na maandalizi ya uhakika.

Tunapaswa kuwapongeza vijana wamejituma kwa uwezo wao bahati haikuwa yao.




Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2

Chapisha Maoni

 
Top