Mchezo huo wa kwanza leo Jumapili katika ligi
hiyo umeshuhudia kikosi cha Stoke City chini
yaaMark Hughes ambacho hakijawahi kupata
ushindi wowote msimu huu kikikomaa na kupata
sare ya bao 1-1.
Manchester United itawabidi wajilaumu wenyewe
baada ya kukosa nafasi nyingi za wazi huku kipa
wa Stoke Grant akionekana ndiye shujaa wa
mchezo huo baada ya kuokoa michomo mingi ya
wazi.
Antony Martial aliyeingia kipindi cha pili kuchukua
nafasi ya Jesse Lingard alitangulia kufunga kabla
ya Joe Allen hajaisawazishia Stoke City kufatia
David De Gea kushindwa kudaka mpira
ulioelekezwa langoni mwake.
Kwa matokeo hayo Stoke City wameongeza pointi
moja na kufikisha pointi 3 baada ya michezo 7
huku United ikifikisha pointi 13.
Like Page ya Facebook Africa Newss Sports Posted: ⚽ Africa News Sports2
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.