0
Mtanzania Mbwana Samatta usiku wa April 13 2017 akiwa na timu yake ya KRC Genk aliingia uwanjani kucheza game yake ya 11 ya Europa League toka waanze hatua ya makundi dhidi ya
Celta Vigo katika uwanja wa Balaidos Hispania.
Mchezo huo ulikuwa ni robo fainali ya kwanza na KRC Genk waliyokuwa ugenini wamejikuta wakipoteza mchezo wao wa kwanza baada ya kucheza game sita mfululizo bila kupoteza katika
mashindano yote, Genk wamefungwa magoli 3-2,
katika historia Genk na Celta Vigo ndio
wamekutana kwa mara ya kwanza.
Magoli ya KRC Genk yalifungwa na Jean Boetius dakika ya 10 na Thomas Buffel aliyeingia akitokea benchi dakika ya 68, kwa upande wa wenyeji magoli yao yalifungwa na Pione Sisto dakika ya
15, Iago Aspas dakika ya 17 na John Guidetti dakika ya 38, kipigo hicho kinailazimu Genk katika
mchezo wa marudiano Luminus Arena April 20 itabidi wapate ushindi wa kuanzia goli 1-0 ili wafuzu nusu fainali.
Kwa upande wa Mbwana Samatta amecheza game hiyo kwa dakika zote 90 na kutimiza jumla ya
dakika 756 alizocheza katika mechi zote 11, akifunga magoli mawili, assist moja na akipiga jumla ya mashuti 7 yaliyolenga goli, Samatta
baada ya kufunga katika mechi 5 mfululizo za Genk leo amecheza game yake ya pili bila kufunga.

Chapisha Maoni

 
Top