Uongozi wa Klabu ya Lipuli 'Wanapaluhengo' umekanusha tetesi za kumsajili Mlinda mlango Peter Manyika Jr Kutoka katika klabu ya Simba.
Mwenyekiti wa klabu hiyo yenye Maskani yake Mjini Iringa, Abuu Changawa 'Majeki', amesema hakuna taarifa Zozote za kumsajili mchezaji yeyote walizozitoa mpaka sasa hivyo hata hilo la Manyika Jr wanashangaa Nani ameliibua.
-Tunafanya Usajili Lakini Bado hatujatangaza nani tumemsajili, hilo la Manyika Jr hatuna la kuzungumza kwa kweli, ni tetesi tu na Tupo kwenye mazungumzona wachezaji Nyota Lakini Hebu subirini taarifa kamili tutawajuza Nani tumemsajili hapo baadae" Alieleza.
Nafasi ya Manyika Jr.
Baada ya Simba kuwasajili Aishi Manula kutoka Azam FC na Emanuel Mseja kutoka Mbao FC kumeifanya nafasi ya Manyika ndani ya kikosi hicho kuwa finyu hivyo kuhusishwa na kujiunga na timu nyingine.
Awali taarifa za Ndani za klabu ya Simba zilisema kwamba wamekusudia kumpeleka mlinda mlango Huyo kwa mkopo katika timu ya Mbao FC.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.