0
Ronaldo aliiongoza Ureno kuibamiza Urusi kwa 1-0 pia Mexico nao waliinyuka Newzealand 2-1 Urusi ikishika nafasi ya tatu kwenye kundi
Baada ya kupamba vichwa vya habari kuhusu mustakabali katika klabu yake kufuatia shutuma za kukwepa kodi, Cristiano Ronaldo ameteka hisia za wengi kwa mara nyingine baada ya kuifungia Ureno goli pekee katika ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji Urusi Kombe la Shirikisho.
Ilimchukua dakika nane tu mshindi huyo wa Ballon d'Or mara nne kuiweka mbele kwa goli moja, shukrani ziende kwa Bernardo Silva na Raphael Guerreiro.
Mchezaji huyo mpya wa Manchester City akishirikiana vema na Guerreiro walimtengenezea mazingira mazuri Ronaldo ambaye hakufanya ajizi na kutikisa nyavu za wapinzani wake.
Ureno kwa kiwango kikubwa walitawala mchezo kipindi cha kwanza, na wangeweza kufunga mabao mawili Ronaldo alipoonyesha ufundi wa kipee lakini mlinda mlango Igor Akinfeev alimudu shuti lake na kudaka.
Akiwa anasubiria siku yake ya kutoa maelezo kuhusiana na kesi inayoendelea kumkabili ya kukwepa kulipa kodi hakika leo Cristiano Ronaldo alikuwa na siku njema.
Baada ya mchezo huo kulipigwa mchezo mwingine kati ya Mexico na Newzealand ambapo hadi mchezo unaisha Mexico waliibuka kidedea kwa bao mbili kwa moja.
Walitangulia Newzealand katika dakika ya 42 kupitia kwa Chris Wood ambapo bao hilo lilidumu kwa kipindi kimoja kwani kipindi cha pili dakika ya 54 Raul Gimenez alisawazisha bao hilo kwa mkwaju mkali sana kabla ya Oribe Pelarta kuifungia Mexico la pili dakika ya 73.
Kwa matokeo hayo ya leo Ureno na Mexico wanakuwa wanalingana alama wote wakiwa na nne nne huku nafasi ya 3 ikishikiliwa na Urusi wenye alama 3 na Newzealand wanaburuza mkia wakiwa hawana alama hata moja na sasa wameaga rasmi mashindano hayo.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top