0
Shirikisho la Soka Nchini TFF, limevunja Ukimya kuhusu mikataba miwili ya Mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbaraka Yusuph Abeidi na kusema kuwa hawafai kuhusishwa na suala hilo kwa kuwa hawahusiki kusaini au kuanika taarifa yoyote ya mchezaji kwani anayehusika ni meneja wa klabu ya husika.
Katika taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya Habari Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas, amesema kuwa hawakuhusika katika kusaini au kuandika mikataba ya mchezaji huyo Kama vile imekuwa ikisambaa mitandaoni.
 Hatujahusika
 -Ndugu zangu kuna mjadala unaendelea, kwenye baadhi ya magroup kuhusu mikataba miwili ya Mchezaji Mbaraka Yussuf Abeidi, Ningependa ifahamike kwamba katika mfumo wa usajili kwa njia mtandao yaani TMS (Transfer Matching System), taarifa huwekwa na meneja wa TMS wa klabu na wala siyo TFF.
TFF wanaweza kusoma taarifa, lakini hawawezi kubadilisha. Kwa hiyo kama mchezaji aliomba nakala ya mkataba kilichotoka kwenye system ni halali mpaka ikithibitika kwamba taarifa zilizowekwa si za kweli.
Na mkataba bila shaka ni kati ya mchezaji na klabu yake hivyo klabu inayochumbia haiwezi ku- conclude uhalali au kutokuwa halali kwa mkataba",amesema Alfred Lucas. Mikataba miwili
Awali Uongozi wa klabu ya Azam ulisema kuwa Mbaraka alipewa mikataba miwili na TFF , moja ya mkataba ukiwa wa mwaka mmoja na mwingine wa miaka mitatu. Mkataba mmoja umesainiwa tarehe 20 Juni 2016 na mwingine ukiwa ni wa tarehe 10 Agosti 2016.
Mara ya pili
Hii ni mara ya pili Mbaraka kujipata katika hali hii tangu ajiunge na "Wakata Miwa hao akitokea Simba ambapo vilabu hivyo viligongana vichwa baada ya kubainika alikuwa na mikataba miwili ambayo majina yake hayakulingana.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top