0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt Harisson Mwakyembe
ameshindwa Kuzuia furaha yake
kutokana na Kiwango kilichooneshwa
na Tanzania katika mchezo wa
kwanza wa Kombe la Mataifa Afrika
dhidi ya Mali.
Mwakyembe amesema ameona na
kujivunia Kiwango bora
kilichooneshwa na Timu ya Taifa ya
Vijana chini ya umri wa miaka 17
Maarufu Kama Serengeti boys na
kusema ana Imani kubwa kuwa Timu
hiyo itafanya vizuri baada ya Sare ya
0-0 na Mali.
-Mashindano yaliyoanza huko Gabon
sisi Tanzania Ndio tulipangwa na timu
ngumu zaidi, Mabingwa watetezi wa
Michuano Hii, Bingwa Anayetaka
kutetea Taji lake, kwa hiyo ulikuwa ni
Mchezo mgumu Sana" Alisema.
Dhidi ya Angola.
Aliongeza kuwa "Nadhani waliopanga
Ratiba walikuwa Wanatoa ahueni kwa
Bingwa ili atupige mabao kama Saba
hivi Kwa bila au kwa moja, ili
waendelee Lakini wamekutana na
Chuma cha pua, sasa subiri Tarehe 18
mchezo utakavyokuwa Kati ya
Tanzania na Angola".
Mwakyembe Amesema michezo miwili
iliyobaki dhidi ya Angola na Niger
Wanaamini Vijana watafanya vizuri na
kuingia hatua ya Nusu fainali na moja
kwa moja wataingia Fainali na
Kuchukua Ubingwa.
Kwa Sasa Msimamo wa Kundi B la
michuano hiyo linaonesha kwamba
Tanzania wanashika nafasi ya 3 na Hii
ni kutokana na Herufi yake ya Kwanza
Kwani Timu ina Alama moja Huku
Tofauti ya Mabao ya kufunga na
kufungwa ikiwa Sawa kwa kila timu.

Chapisha Maoni

 
Top