(TFF), limetangaza Makundi ya Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) ambapo
timu saba zitapangiwa katika kila
kundi kwenye michuano hiyo
itakayoanza Mei 28, mwaka huu.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika
katika vituo vya Lindi, Songwe, Tabora
na Kahama mkoani Shinyanga Huku
Ratiba za mechi kwa kila kituo
itatolewa Mei 22, mwaka huu.
Hata hivyo, michuano ya RCL
imechelewa kuanza baada ya baadhi
ya timu kushindwa kukamilisha vigezo
vya ushiriki ikiwa ni pamoja na kulipia
ada ya ushiriki kwa wakati, leseni za
wachezaji kwa wakati pamoja na
kuwasilisha usajili kwa wakati,
ambapo sasa Mwisho Utakuwa ni Mei
18 Mwaka huu kukamilisha vigezo
hivyo.
Tayari Makatibu wa Mikoa
wamejulishwa hilo tangu Mei 5,
mwaka huu, lakini sasa kwa timu
ambazo hazitakamilisha taratibu za
kulipia ada au leseni za wachezaji
itaondolewa kwenye mashindano.
Makundi.
Kundi A litakuwa Mkoa wa Lindi
ambako kutakuwa na timu za
Shupavu FC ya Morogoro, Silabu FC
ya Mtwara, Mbinga FC ya Ruvuma,
Politan ya Dar es Salaam, Makambako
Heroes ya Njombe, Ambassador ya
Shinyanga na New Generation ya
Mtwara.
Kundi B litakuwa Mkoa wa Songwe
ambako timu za kituo hicho ni
Kisarawe United ya Pwani, Moto Chini
FC ya Mtwara, Makanyagio FC ya
Katavi, Makumba ya Dar, Boma FC ya
Mbeya, Real Mojamoja ya Iringa na
Sahare All Stars ya Tanga.
Kundi C litakuwa Kituo cha Mkoa wa
Tabora ambako kutakuwa na timu za
Nyanza FC ya Manyara, Nyundo FC ya
Kigoma, Eleven Stars ya Kagera,
Bodaboda FC ya Arusha, Stand
Misuna ya Singida, Majimaji Rangers
ya Lindi na Area C United ya
Dodoma.
Kwa upande wa Kundi D ambalo kituo
chake ni Kahama mkoani Shinyanga,
kutakuwa na timu za Dar City ya Dar,
Buseresere ya Geita, Ndovu Sports ya
Mwanza, Usamala FC ya Simiyu,
Baruti FC ya Mara, Green FC ya
Songwe na Msange FC ya Tabora.

Chapisha Maoni