0
Licha ya winga wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe, kupongeza juhudi ya kamati ya usajili ya timu hiyo, iliyo chini ya Zacharia Hans Poppe,ila amesikitishwa na viongozi kumwachia Ibriham Ajibu, asaini Yanga miaka miwili.
"Unapozungumzia Simba au Yanga, lazima uangalie wachezaji ambao walikuwa mzizi wa timu, mtu kama Ajibu, Mkude, Tshabalala na wengineo (Simba),walitakiwa wamalizane nao mapema ndipo wawaongezee wengine ambao wanawatoa sehemu nyingine,"anasema
Ulimboka anasema Simba, wanatakiwa kuumiza akili namna ya kuhakikisha wanampata mbadala wa Ajibu na ikiwezekana na aliyemzidi uwezo vinginevyo itaendelea kuwaumiza mashabiki wao.
"Mfano Amissi Tambwe ambaye ndiye alikuwa mwiba kwao namna ambavyo alikuwa anafunga na huku Simba, wakikosa mfungaji sahihi mara afunge winga mara beki,wajipange, watulize akili, wasifanye kwa papara huku wakijua mwakani wanacheza michuano ya kimataifa,"anasema Ulimboka.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top