0
Baada ya kuipa mafanikio makubwa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameangusha bomu akiuambia uongozi wa klabu hiyo anataka kuondoka.
Ronaldo ametoa kauli hiyo akiwa kwenye kikosi cha Ureno kinachoanza michuano ya Kombe la Mabara nchini Russia kesho.
Mitandao mbalimbali ya soka imemkariri Ronaldo akiangusha bomu hilo kwa Real Madrid na kuiamsha Manchester United, ambayo inaweza kujaribu kumrudisha.
Ronaldo, mshindi mara nne wa tuzo ya ubora, Ballor d'Or ameeleza dhamira ya kutaka kurudi Old Trafford kabla ya kustaafu soka, akieleza kuwa ni kutokana na klabu hiyo kushindwa
kumlinda dhidi ya mamlaka za mapato.
Real Madrid imejibu ikiiambia Man United iandae Pauni 160 milioni, limeeleza gazeti la Marca.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top