0
Beki wa Yanga, Haji Mwinyi amefikia makubaliano na mabosi wa mabingwa hao wa Tanzania Bara wa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.
Mwinyi amesema sababu ya kusaini kwake ni maboresho aliyofanywa katika kipengele cha mshahara wake.
"Keshokutwa Jumatatu, nakuja Dar es Salaam kusaini mkataba wa miaka miwili ya kuitumikia Yanga kwa mara nyingine tena, kila kitu kipo sawa kwa sasa, kilichobakia ni kusaini tu,"alisema
Mwinyi, alisema baada ya kusaini mkataba huo akili yake itabakia kujiandaa na msimu ujao kwani hatakuwa chini ya presha ya kutojua atacheza wapi kwa madai amejihakikishia kuvaa uzi wa njano.
Akizungumzia kuhusiana na ugeni wa Ibrahim Ajibu, aliyesaini mkataba wa miaka miwili Yanga, kwamba kama kuna bonge la dili walilopiga mabosi zake ni hilo kwani wamepunguza makali ya Simba, msimu ujao.
"Kama kuna mchezaji alikuwa anatupa presha ndani ya Simba ni Ajibu, viongozi wamesajili bonge la mchezaji, kikubwa nimwambie mchezaji mwenzangu, karibu Yanga, kwenye timu yenye mafanikio ya kuchukua mataji ya ligi kuu,"alisema Mwinyi.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top