0
Nahodha wa Timu ya Simba Jonas Mkude amepuzilia mbali madai kuwa anahama klabu hiyo na kusema baada ya mkataba wake nao kumalizika na kusema kuwa mazugumzo kuhusu kusaini mkataba mpya na Simba umeanza.
 Katika mahojiano na kituo cha Radio One,Mkude amethibitisha kuwepo kwa mazugumzo hayo na kuelezea matumaini yake kuwa mambo yatakuwa Sawa.
Mchezaji wa Simba
-Naondoka vipi simba wakati bado nilikuwa ndani ya Simba na bado niko ndani, mkataba kweli umeisha ndio lakini mwisho wa siku Nina makubaliano na Simba na bado ninaendelea na mazugumzo na wakubwa wangu",amesema Kiungo huyo.
 Kuhusu mazugumzo yake na klabu hiyo yamefikia hatua gani Mkude amesema yamefikia pazuri.
Mazugumzo
-Mazugumzo yako vizuri na mwisho wa siku Mwenyezi Mungu atajalia,ameongeza Mkude.
Aidha kumekuwa na taarifa za kuhama kwa Kiungo huyo ambayo inadaiwa amekuwa akiitisha dau kubwa ili kubaki na Simba msimu ujao jambo Mchezaji huyo hakutaka kulizungumzia akidai ni tetesi.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top