0
Beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomari ametajwa katika orodha ya wachezaji wanakiwa na Simba msimu huu.
 Simba tayari imesajili wa wachezaji kadhaa na kuwatangaza wawili Jamal Mwambeleko na Yusuph Mlipiliiki huku nyota wao John Bocco aliyetokea Azam akifungiwa kabatini.
Taarifa kutoka katika uongozi wa Simba zinadai kuwa kwa sasa wapo katika mazungumza Shomari aliyemaliza mkataba wake na Mtibwa Sugar.
Shomary alikiri kufanya mazungumzo na viongozi wa Simba; "Tumezungumza tu na wameniahidi watanipigia simu wakimaliza kujadiliana, hivyo nawasubiri wao kama watarudi kweli na kufikia makubaliano ya mwisho nitasaini wasiporudi napo hakuna tatizo lolote.
"Mimi ni mchezaji, mkataba wangu na Mtibwa Sugar umemalizika bado sijaambiwa jambo lolote na viongozi wangu wa Mtibwa kuhusu mkataba mpya, hivyo popote nitakaporidhishwa na ofa nitasaini hata hapa kwani si timu mbaya kwangu," alisema Shomary.

Chapisha Maoni

 
Top