Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umesema kuwa hauna taarifa za Mshambuliaji wao Mbaraka Yusuph kuhamia Timu ya Azam na kuwa kama kuna Timu yoyote inayohitaji huduma za mchezaji huyo Kufuata taratibu zinazostahili kwa kuwa Mbaraka ni mchezaji wao na ana mkataba wa miwili na Wakata Miwa hao.
Akitoa ufafanuzi wa usajili huo ambao ulivuja mitandaoni Jana usiku Mratibu wa Kagera Sugar Fc Mohamed Hussein amesema kuwa klabu hiyo haijapokea ofa yoyote kuhusu Mbaraka yusuph kufikia sasa.
Hatujapokea ofa
-"Sisi mpaka sasa hatujapata ofa yoyote kuhusu Mbaraka tunasikia sikia tu tetesi mara kasaini Simba mara Yanga na jana tunasikia Azam, na sisi hatuna haja ya kumuuliza maana yeye anajua wajibu wake anajua kama ana mkataba na Kagera Sugar ni vyema akiviambia vilabu vinavyo mhitaji kua ana mkataba"amesema Hussein.
Kufuata utaratibu
Mratibu huyo ameendelea na kusema kuwa vilabu vinavyomuhitaji Mbaraka kutumia utaratibu unaofaa kwa kuwa bado ni mchezaji halisi wa Kagera Sugar.
- Mbaraka Yusuph ana mkataba na Kagera Sugar bado ana miaka miwili mbele maana alisaini miaka mitatu, tulimpa mkataba wa muda mrefu baada ya kumaliza mgogoro na Simba Sc,kama kuna Klabu inamhiitaji ni vyema kwanza ikaja kuongea na Kagera Sugar kabla ya kuongea na mchezaji ili na sisi tuseme nini tunahitaji huo ndo utaratibu, kama kuna Klabu itakwenda kinyume na hivyo Sheria itachuku mkondo wake kama ilivyo kua kwa kesi ya Hassan Kessy",amesema Hussein.
Mabao 12
Mbaraka ambaye msimu uliopita amekuwa na msaada mkubwa kwa Wakata Miwa hao akifanikiwa kuwafungia mabao 12 amekuwa akiwindwa na vilabu kutokana na kuimarika kwa kiwango chake.
Chapisha Maoni