Usiku wa June 24, 2017 mshambuliaji wa zamani wa Simba Mganda Emanuel Okwi aliwasili kimya kimya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage nyerere Dar es Salaam ili kujiunga na wekundu wa Msimbazi Simba.
Okwi alipokelewa na makamu wa Rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu na kutotaka kuongea chochote na waandishi wa habari.
Okwi ambaye anarudishwa kujiunga na Simba kwa mara ya Tatu, alitazamiwa kuwasili asubuhi ya siku hiyo Lakini kutokana na sababu zisizotajwa alichelewa kufika na kuingia usiku wa saa Tano kasoro.
Miaka Miwili.
Taarifa zinasema kwamba Okwi ametua nchini ili kukamilisha uhamisho wake wa miaka miwili kuitumikia Simba ambayo mwakani itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kama Okwi akikubaliana na Simba atakuwa amejiunga na Timu hiyo kwa Mara ya Tatu, Kwani alijiunga Mwaka 2009 Kabla ya kurejea tena Mwaka 2013 na Hii sasa itakuwa ni Mara ya Tatu.
Mshambualiaji Huyo wa timu ya Taifa ya Uganda anatokea timu ya SC Villa ambapo katika mechi Chache alizocheza msimu uliopita alifanikiwa kufunga Mabao 7.
Chapisha Maoni