0
Mabingwa wa Zamani wa Kenya Gor Mahia wameanza vyema michuano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwachabanga Timu ya Soka ya Jang'ombe Boys kutoka Zanzibar kwa Mabao 2-0 katika mfulululizo wa michuano hiyo inayoendelea kwenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Gor Mahia walijipatia bao la kwanza Mnamo dakika ya 63 kwa Kichwa mujarabu cha Medy Kagere kilichomshinda mlinda mlango wa Jang'ombe Boys Ruga Haroon.
Medy Kagere Akaipatia tena bao la Pili Timu ya Gor Mahia kwa mkwaju wa penati Mnamo dakika ya 82 ya mchezo huo baada ya Mlinzi wa Jang'ombe Boys kuunawa Mpira akiwa ndani ya 18.
Kashikashi za Kagere.
Kabla ya kufunga mabao hayo Kagere alikuwa Mwiba Mkali kwenye Lango la Jang'ombe Boys Kwani katika dakika ya 42 akiwa yeye na kipa Ruga Hood alishindwa kuukwamisha Mpira huo Wavuni na kuutoa sentimita Chache langoni mwa Jang'ombe Boys.
Aidha Mapema kabisa katika dakika ya 25 ya mchezo huo
Gor Mahia walipoteza nafasi ya kupata bao la kuongoza, shuti la Medy Kagere likapaa juu na kuwapa ahueni Jang'ombe Boys.
Nusu fainali.
Kwa ushindi huo Gor Mahia wanaingia moja kwa moja katika hatua ya Nusu fainali itakayopigwa Ijumaa ya Juni 9 mwaka huu, wakiisubiri Mshindi wa mchezo kati ya Nakuru All Stars na Simba SC ambaye Ndiye watakayekutana Naye katika mchezo huo.

Chapisha Maoni

 
Top