0
Nakuru All Stars inayoshiriki Ligi daraja la pili nchini Kenyaimetinga nusu fainali ya michuano ya Sportspesa Super Cup baada ya kuwatoa Timu ya Soka ya Simba ambao ni mabingwa wa kombe la Shirikisho Tanzania Bara kwa ya jumla ya penati 5-4 baada ya Dakika 90 kumalizika Kwa Sare ya 0-0.
Aidha Mchezo huo ulikuwa wa kiufundi kwa kila upande huku timu zote zikionekana kujilinda hadi mapumziko Simba 0-0 Nakuru All Stars.
Mabadiliko
Kipindi cha pili mkocha wa timu zote wamefanya mabadiliko huku wakijaribu kuimarisha safu za ushambulizi na ulinzi lakini hazikuonekana kufua dafu huku timu zote zikishindwa kutumia nafasi chache za wazi walizozipata.
Dakika tisini za mchezo huo zimehitimishwa kwa timu zote kushindwa kuona lango la wapinzani na kulazimika kutumika hukumu ya matuta ili kupata mshindi.
Daniel Agyei
Aidha mlinda mlango wa timu ya Simba Daniel Agyei alikosa penati muhimu na kutoa nafasi kwa Nakuru All Stars kufuzu hatu ya Nusu Fainali ya michuano hiyo ambayo inaendelea kawenye uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Simba wanakuwa timu ya tatu kutoka Tanzania kuyaaga mashindano hayo wakati Nakuru All Star wakitarajiwa kukutana na Gor Mahia katika nusu fainali ya pili ya michuno hiyo.

Chapisha Maoni

 
Top