0
Real Madrid wanapanga kusitisha mazungumzo kuhusu kumuuza Alvaro Morata kwenda Manchester United, kufuatia Cristiano Ronaldo kusema anataka kuondoka Spain, imeripoti tovuti ya AS.
Ronaldo aliushangaza ulimwengu wa soka siku ya Ijumaa baada ya watu wake wa karibu kusema anataka kuondoka Spain.
Hatua ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kutaka kuondoka Bernabeu huenda ikaathiri mustakabali wa Alvaro Morata, ambaye anasakwa na Manchester United.
Real Madrid na Manchester United walikuwa kwenye mazungumzo ya kina kuhusiana na uhamisho wa Morata, na taarifa zinasema tayari walikuwa wamefikia makubaliano.
Mkutano kati ya vilabu hivyo viwili wa kukamilisha mkataba huo uliokuwa ufanyike wiki ijayo, sasa huenda ukasogezwa mbele, kwa kuwa mabingwa hao wa Ulaya hawatotaka kumuuza Morata ikiwa Ronaldo ataondoka.
(Chanzo: Transfer Centre Live! ya
SkySports.com )

Chapisha Maoni

 
Top