ACHANA na usajili wa kipa Shaaban Kado, Mtibwa Sugar, imeonyesha msimu huu haina mzaha baada ya kunyakua nyota wa zamani wa Simba na Yanga, akiwamo Danny Lyanga, aliyekuwa akicheza soka la kulipwa Fanja FC ya Oman.
Lyanga aliwahi kutamba Simba kabla ya kwenda Umangani na tayari amejiunga na Mtibwa sambamba na akina Kado na kiungo wa zamani wa Yanga, Hassan Dilunga aliyesaini mkataba wa miaka miwili juzi Jumapili.
Mbali ya Lyanga na Dilunga, pia Mtibwa imemnasa straika wake wa zamani, Mohammed Mkopi.
Mwanaspoti imewashuhudia nyota hao wakipiga tizi Uwanja wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam chini ya Kocha Zuberi Katwila.
“Mtibwa ni nyumbani, ni sehemu ambayo imenifanya nijulikane kisoka, hivyo kusajiliwa tena si kitu cha ajabu, nimerudi kuleta mapinduzi,” alisema Kado aliyewahi kuzidakia Yanga na Coastal Union kabla ya kutua Mwadui kwa misimu miwili iliyopita.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni