Mshambuliaji Javier Hernandez amekamilisha uhamisho wake wa pauni16milioni kutoka Bayer Leverkusen kwenda West Ham na kuwa mchezaji ghali zaidi kusajili katika historia ya klabu hiyo.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United atakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi historia ya Hammers akipokea mshahara wa pauni140,000 kwa wiki katika miaka mitatu.
Hernandez anaungana na wachezaji wengine wapya waliosajiliwa na West Ham, akifuatiwa na Joe Hart, Marko Arnoutovic na Pablo Zabaleta kwenye Uwanja wa London.
Akizungumzia uhamisho wake Hernandez alimbia tovuti ya klabu hiyo: “Nimefurahi kujiunga na West Ham United.
“Kwangu mimi, Ligi Kuu England ni moja ya ligi bora duniani na wakati nafasi ilipotekea, sikutaka kuipoteza.
“Haukuwa uamuzi mgumu. West Ham ni klabu yenye historia kubwa na yenye malengo, msimu huu utaona aina ya wachezaji iliyowasajili wote wanaonekana ni wakiwango cha juu.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni