Eden Hazard amemwambia Rais wa Real Madrid, Florentino Perez afahamu tu hawezi kuiacha Chelsea ikiwa kwenye hali ya sintofahamu.
Hazard anaripotiwa kuwaambia Real Madrid kama wanataka kumsajili kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi basi wafanye haraka sana kabla ya muda haujakwisha ili kuwafanya Chelsea kupata nafasi ya kusajili mbadala wake.
Mbelgiji huyo ametoa tahadhali tu akidai hawezi kuondoka huko Stamford Bridge kama The Blues hawatakuwa kwenye wakati mzuri wa kupata mchezaji wa kuziba pengo lake.
Dirisha la usajili wa majira haya ya kiangazi unatarajiwa kufungwa Agosti 9, hivyo kazi ni kwa Los Blancos kuhakikisha wanakamilisha usajili wa Hazard ili kutoa nafasi ya Chelsea kufanya usajili wa mbadala wake.
Mpango wa Chelsea ni kumsajili winga wa Manchester United, Mfaransa Anthony Martial. Chelsea inahitaji Euro 200 milioni kwenye mauzo ya Hazard kiasi ambacho Perez anakiona kimezidi sana.
Lakini sasa staa huyo wa Ubelgiji anaonekana kumlazimisha rais huyo wa Bernabeu kufanya haraka kuinasa saini yake.
Chapisha Maoni