0
Mshambuliaji Harry Kane na Mohamed Salah wametajwa katika orodha ya wachezaji kumi wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifia 2018, huku Neymar akiachwa.
Nahodha wa England, Kane na nyota wa Liverpool, Salah wametaja katika orodha ya fifa iliyotolewa leo Jumanne ya wachezaji hao 10, waliopitishwa na jopo la na wachezaji wa zamani wenye mafanikio makubwa kama Kaka, Didier Drogba na Frank Lampard, na wengine.
Bingwa wa Kombe la Dunia Ufaransa, ametoa wachezaji watatu katika orodha hiyo Antoine Griezmann, Kylian Mbappe na beki Raphael Varane pamoja mshindi wa mpira wa dhahabu Luka Modric.
Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard pamoja na kiungo wa Manchester City, Kevin De Bruyne wameungana na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi katika kinyang’anyiro hicho.
Hata hivyo, hakukuwa na nafasi Neymar, pamoja na Mbrazil huyo kufunga mabao 28, katika msimu wake wa kwanza Paris Saint-Germain.
Neymar alishindwa kuisaidia timu yake ya taifa kufuzu kwa robo fainali ya Kombe la Dunia baada ya Brazil kuchapwa na Ubelgiji.
Baada ya orodha hiyo kutoka manahodha wa timu za taifa, makocha, mashabiki na wanahabari wataanza kupiga kura za kuchagua mchezaji bora hadi Agosti 10.
Baada ya hapo Fifa itatangaza wachezaji watatu wa mwisho ambao kati yao ndipo atatangazwa msindi mmoja katika hafla itakayofanyika London hapo Septemba 24.

Chapisha Maoni

 
Top