0
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amejumuishwa miongoni mwa makocha 11, waliotajwa kuwania tuzo ya Kocha bora wa mwaka Fifa kwa wanaume.
Klopp amepewa nafasi hiyo ya kuwania tuzo hiyo kutokana na mafanikio aliyoyapata Liverpool, ikiwemo kuiwezesha kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, 2017-18.
Makocha wengine anaochuana nao ni pamoja na Kocha Massimiliano Allegri (Juventus), Stanislav Cherchesov (Russia), Zlatko Dalic (Croatia), Didier Deschamps (Ufaransa), Pep Guardiola (Manchester City), Roberto Martinez (Ubelgiji), Diego Simeone (Atletico Madrid), Gareth Southgate (England), Ernesto Valverde (Barcelona) na Zinedine Zidane (Real Madrid).
Kocha bora atatangazwa katika hafla itakayofanyika jijini London, Uingereza Septemba 24 mwaka huu, tuzo ambayo hupigiwa kura na makocha wa timu za Taifa, manahodha pamoja na waandishi wa habari.

Chapisha Maoni

 
Top