Klabu ya Yanga imeanza kuziba mapengo ya watendaji wake kwa kumteua Omary Kaaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu akichukua nafasi ya Charles Boniface Mkwasa.
Awali Kaaya alikuwa ofisa masoko wa klabu hiyo kabla ya Bodi ya wadhamini na kamati tendaji kumteua kukaimu nafasi ya Mkwasa.
Ofisa habari wa Yanga, Dismas Ten amesema uteuzi huo ulifikiwa katika kikao cha dhararu kilichofanyika jana baada ya makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Clement Sanga kutanagza kujiuzuru jana mchana.
"Tuko katika mashindano ya kimataifa na kipindi cha usajili, hivyo kutokana na kinachoendelea ilikuwa lazima tuwe na katibu mkuu ambaye atasimamia mambo hayo," alisema Ten.
Chapisha Maoni