Apple Yathibitisha Kununua Bidhaa za Beats Electronics Kwa Dola Bilioni 3
Baada ya ukimya wa muda mrefu tangu kuwe
na habari kuwa kampuni ya Apple imepanga
kununua headphones zinazotengenezwa na
Beats Electronics ‘Beat by Dre’, Jana kampuni
hiyo imethibisha mpango huo.
CEO wa Apple, Tim Cook amethibisha kuwa
kampuni yake imeshafanya mazungumzo na
Jimmy Lovine na Dr Dre na kwamba
makubaliano yao ni kuwalipa Lovine na Dre
kiasi cha dola bilioni 3.
Cook ameeleza uhusiano kati ya kampuni yake
na Lovine na Dre akitolea taswira ya
mahusiano ya wawili wanaojuana kwa miaka
mingi na sasa wanaishia kwenye ndoa
itakayokuwa imara. “Tumekuwa tukiwafahamu hawa jamaa muda
wote, tumechumbiana, tumekuwa na uhusiano
imara na sasa tunafunga ndoa. Uhusiano huu
umeanza muongo mmoja uliopita, kwa hiyo
tunafahamu kuwa kuna utamaduni unaofit
pande zote mbili.” Amesema Cook kwenye
maelezo yake.
Kati ya dola bilioni 3, Apple watalipa fedha
taslim dola bilioni 2.6 na kiasi kingine
kitakuwa katika share ya bidhaa.
Lovine na Dre wote watapewa nafasi ya
kuratibu katika kampuni ya Apple kwa upande
wa muziki japo Cook hakueleza wazi wajibu na
kazi watakayokuwa wakiifanya.
Manunuzi haya yanakuwa kati ya makubalino
makubwa zaidi katika historia ya kampuni ya
Apple kwa miaka 38.
Mchongo huu utakapokamilika, Dr Dre
atakuwa anatembea kifua mbele ambapo
Forbes itabadili orodha ya majina ya wana hip
hop matajiri zaidi duniani na kumfanya Dr Dre
kuwa mwana hip hop wa kwanza kuwa
bilionea.
Chapisha Maoni