MUTHARIKA RAIS MPYA MALAWI
Mgombea wa Chama cha upinzani nchini
Malawi Peter Mutharika ametangazwa
mshindi katika uchaguzi wa urais uliozua
utata.
Mutharika wa Chama cha Democratic
Progressive Party amepata asilimia 36.4 ya
kura, imetangaza tume ya uchaguzi nchini
humo.
Rais anayeondoka madarakani Joyce Banda
amedai uchaguzi huo ulivurugwa.
Tume ya uchaguzi ya Malawi (MEC)
iliomba siku 30 za ziada ili kura
zihesabiwe upya kabla ya kutangaza
matokeo.
Hata hivyo, Mahakama Kuu ilitupilia
mbali ombi hilo na kutoa amri ya matokeo
kutangaza siku ya Ijumaa.
"Sheria iko wazi, hakuna kuongeza
muda," amesema Jaji Kenyatta Nyirenda.
Bwana Mutharika ni ndugu yake Rais
Bingu wa Mutharika aliyefariki dunia
mwaka 2012. Peter Mutharika alikuwa
Waziri wa mambo ya nje wakati ndugu
yake akiwa rais.
Chapisha Maoni