UKATILI WA AJABU: Baba ampaka mwanae pilipili machoni, amchapa viboko, ngumi na mateke hadi kufa
JESHI la Polisi mkoani Geita, linamshikilia
William Kibyala (40), mkazi wa Kijiji cha Misiri,
Kata ya Bugarama, Wilayani Geita kwa kosa la
kumpaka pilipili machoni mwanae John Wiliam
(4), na kumchapa viboka sehemu mbalimbali
za mwili wake hadi kufa.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Joseph
Konyo, amethibitisha Jeshi hilo kumshikilia
mtuhumiwa huyo muda mfupi baada ya tukio
hilo lililotokea Mei 23, 2014 ambapo
amesema mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani
mara baada ya upelelezi kukamilika.
“Mtoto huyu alifariki baada ya kupewa adhabu
na Baba yake mzazi kwa kupigwa na kupakwa
pilipili, huyu mtuhumiwa tunamshikilia hadi
sasa na uchunguzi zaidi wa tukio hili bado
unaendelea kwahiyo kwa taarifa nyingine
tutawaambia ili muujulishe Umma wa
watanzania kupitia kwenu na vyombo vingine
vya habari” alikaririwa Konyo katika
mahojiano na mwandishi wetu Aidha, alisema Baba wa mtoto huyo anadaiwa
kufanya ukatili huo baada ya kumtuhumu
mtoto huyo kukataa kumfungulia mlango
wakati alipotoka matembezini usiku wa
manane.
Baadhi ya wananchi wanaoishi katika Kijiji
hicho wamedai kuwa mtoto huyo alifariki
baada ya kuchapwa fimbo mwili mzima,
kupigwa ngumi na mateke, kisha kupewa
adhabu ya kukimbia riadha ya kuzunguka
nyumba yao usiku wa manane kabla ya kifo
chake.
Mmoja wa mashuhuda hao, Irine Kaijage,
amesema baada ya mtoto huyo kumaliza
adhabu hiyo alipakwa pilipili machoni na
makalioni hali iliyosababisha mtoto huyo
kuzidiwa na kupoteza maisha Mei 24, 2014
jioni.
Mmoja wa watoto wa Mzazi huyo, Shija
William, alisema mdogo wao alikuwa akipewa
adhabu hiyo mara kwa mara na Baba yao kwa
madai kwamba Mama yao alimbambikizia
mdogo wao kwani yeye hakumzaa.
Chapisha Maoni