Kifo cha Recho Haule kimemfanya Jackline Wolper afute mipango yake ya kuzaa akihofia kufa
Staa wa kike wa filamu za kibongo,
Jackline Wolper amefunguka kuwa kwa
sasa hana wazo kabisa la kubeba mimba
kwani staili ya kifo cha Recho Haule
inamuumiza sana kichwa....
Ingawa Wolper anaamini kuwa ni wajibu
wa kila mwanamke kuzaa, lakini aina ya
kifo ambacho rafiki yake kipenzi Recho
amekufa nacho kimekuwa ikimtesa sana
moyoni na kumfanya afute mipango yake
ya kuzaa akihofia kufa.
"Najua ni wajibu wetu kuzaa, lakini
nimekuwa na hofu kubwa ya kushika
mimba sababu mimi ni muoga sana wa
kuzaa, na kila nikikumbuka kifo cha Recho
ndo kabisaa nazidi kuchanganyikiwa.
"Napenda sana kuwa na mtoto, lakini si
leo wala kesho. Nahitaji muda wa kujenga
ujasiri mpya, lakini kama itatokea
ntajitahidi kuvumilia," alisema
Chapisha Maoni