0
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara leo wameanza vyema mbio za kubakiza taji lao, baada ya kuichapa Polisi Morogoro mabao 3-1 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Ushindi huo unaomfuta machozi kocha
Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya kufungwa 3-0 na Yanga SC katika mchezo wa Ngao ya Jamii ulitokana na mabao ya Didier
Kvumbangu mawili na Aggrey Morris.
Azam walikwenda kupumzika wakiwa
wanaongoza mabao 2-0, Kavumbangu
akianza kufunga dakika ya 14 akiunganisha pasi ya Kipre Tchetche katikati ya beki na kipa wa Polisi.Beki Aggrey Morris akaipatia bao la pili Azam FC dakika ya 23 aliyemalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Kipre Tchetche kufuatia beki Gardiel Michael kuchezewa rafu na Bantu Admin.

Baada ya mabao hayo mawili ya haraka
haraka, kocha wa Polisi Morogoro,
Mohammed Adolph ‘Rishard’ alimpumzisha kiungo Bantu Admin na kumuingiza James Mganda.

Mabadiliko hayo kidogo yaliituliza Polisi na kuanza kufika kwenye lango la Azam, ingawa hawakufanikiwa kupata bao hadi dakika 45 za kwanza zilipokamilika.

Mshambuliaji wa zamani wa Simba SC, Danny Mrwanda alidhibitiwa vikali na mabeki wa Azam leo.
Kipindi cha pili, Azam FC ilirudi vizuri na
kusukuma mashambulizi mfululizo langoni mwa Polisi, lakini mshambuliaji Kipre Tchetche alikosa mabao matatu ya wazi.
Nahoda Bakari aliipatia bao Polisi dakika ya 60 baada ya kuanzishiwa kona fupi na kumtungua kwa shuti la umbali 22 kipa Aishi Manula.

Didier Kavumbangu aliifungia bao la tatu
Azam FC dakika ya 90 akimalizia krosi ya Farid Malik.


Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Himid Mao/Khamis Mcha ‘Vialli’ dk72, Mudathir Yahya, Didier Kavumbangu, Kipre Tchetche/
Farid Malik dk72 na Salum Abubakar.


Polisi Moro; Tony Kavishe, Rogeri Fred,
Simon Fanuel, Ally Feruzi Telu, Lulanga
Mapunda, Said Jella, Bantu Admin/James Mganda dk22, Nahoda Bakari/Suleiman Kassim ‘Selembe’ dk65, Danny Mrwanda, Machaku Salum na Nicholas Kabipe/Edgar Charles dk65.

Chapisha Maoni

 
Top