YANGA SC imeanza kwa kipigo cha mabao 2-0 Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro mshambuliaji Genilson Santana
‘Jaja’ akikosa penalti.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Dominick Nyamisana wa Dodoma,
aliyesaidiwa na Ferdinand Chacha wa Mwanza na Milambo Tshikungu wa Mbeya, hadi mapumziko tayari Mtibwa Sugar walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wa
zamani wa Simba SC na DC Motema Pembe ya DRC, Mussa Hassan Mgosi dakika ya 16 aliyemalizia pasi ya kichwa ya Ame Ali na kumuwahi kipa Deo Munishi ‘Dida’ aliyetokea vizuri kutaka kudaka.
Baada ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo kuendelea.
Baada ya bao hilo, nyuki wakaingia uwanjani jambo lililosababisha wachezaji walale chini kwa dakika mbili, kabla ya wadudu hao kuondoka na mchezo kuendelea.Almanusra Genilson Santana ‘Jaja’
aisawazishie Yanga SC dakika ya 32 baada ya kuunganisha vizuri kwa kichwa kona ya Haruna Niyonzima, lakini Hassan Ramadhani akauokoa ukiwa unaelekea nyavuni.
Dakika ya kwanza tu ya kipindi cha pili,
Yanga SC walipata penalti baada Salim
Mbonde kuunawa mpira kwenye eneo la
hatari, lakini kipa Said Mohamed Kasarama akapangua kwa mguu mkwaju wa Jaja.
Dakika ya 47, Simon Msuva aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Hamisi Kiiza
‘Diego’aliifungia Yanga SC bao, lakini refa akasema aliotea. Dakika ya 49 tena, Mrisho Ngassa alifunga bao lakini refa akasema aliotea pia.
Dakika ya 67, Simon Msuva alivamia langoni mwa Mtibwa na kutoa vitu vilivyokuwa chini upande wa nyavu kubwa na kukimbia navyo huku akikimbizwa na kipa Said Mohamed
Kasarama kabla ya kuvitupa nje.
Dakika ya 82 mpishi wa bao la kwanza, Ame Ali aliifungia Mtibwa bao la pili baada ya kufanikiwa kuwahadaa mabeki wawili wa kati wa Yanga SC, Nadir Haroub ‘Cannaaro’ na Kevin Yondan kisha kumtungua Dida kufuatia
pasi nzuri ya Hassan Ramadhani.
Yanga SC iliathiriwa na mabadiliko
iliyoyafanya dakika za mwishoni kumtoa
Mbuyu Twite aliyekuwa mhimili wa safu ya ulinzi na kuingiza mshambuliaji, Said
Bahanuzi.
Kocha wa Yanga SC, Marcio Maximo ambaye alimfundisha kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime alipokuwa Taifa Stars alikuwa mnyonge baada ya meci hiyo.
Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Said
Mohammed, Hassan Ramadhani, David
Luhende/Majaliwa Shaaban dk64, Salim
Mbonde, Andrew Vincent, Shaaban Nditi, Ali Shomary, Muzamil Yassin, Ame Ali, Mussa.Mgosi/Vincent Barnabas dk50 na Mussa Nampaka/Dickson Daud dk72.
Yanga SC; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua/Omega Seme, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite/Said Bahanuzi dk72, Hassan Dilunga, Haruna
Niyonzima, Genilson Santana ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Hamisi Kiiza/Simon Msuva dk46.
Chapisha Maoni