September 12 2014 Mahakama ya Pretoria nchini Afrika Kusini ilimpata Oscar Pistorius na hatia ya
kumuua mpenzi wake bila kukusudia kwenye siku ya Wapendanao February 14 2013.
Baada ya maamuzi hayo kutangazwa, familia ya binti aliyeuwawa Reeva Steenkamp imekasirishwa
na uamuzi wa jaji wa kesi hiyo kwani mtoto wao alikufa kifo kibaya na ndio maana hawajaamini kilichotokea kwamba Jaji ameamini ushahidi wa
Pistorius kuwa alimpiga risasi binti huyo kwa kudhani ni mwizi.
Mwanariadha Oscar ataendelea kuwa nje kwa dhamana kwa mujibu wa BBC mpaka hukumu yake itakapotolewa mwezi ujao.
Chapisha Maoni