Muigizaji wa filamu za Kiswahili, Steve Nyerere aliyekuwa Rais wa Klabu ya Bongo Movie Unity ameamua kujiuzulu nafasi hiyo.
Steve ameeleza uamuzi wake kupitia Instagram bila kutoa sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake.
“Napenda kuwashkulu ndugu zangu wote wasaniii wenzangu kaka zangu mama zangu rafiki zangu
mimi pamoja na family yangu nimeamua
kujiuzuru uongozi wa bongo move nabaki kuwa mwanachama wa kawaida naimani tulifurahi
pamoja tukauzunika pamoja na daima tutakuwa pamoja.”
Uamuzi wa Steve Nyerere umepokelewa kwa hisia tofauti na wapenzi wa filamu za kitanzania ambao wengine wamemtaka kutofanya hivyo huku
wakitaja ‘majungu’ na kusemwa kama chanzo cha yote.
“Khaaaaaaa asa @stevenyerere2 kujihuzur sio suluhisho la tatizo kaanza willy umefata ww sasa c kamat nzima itajiuzur!?? Why mnashindwa
kukaa km wasanii mkasuluhisha penye makosa mambo yakaendelea? Majungu yapo kila sehem kusemwa kupo kila sehem @stevenyerere2
mnapoelekea bongomovie kila mtu atakaa mwenyewe wallah.” Ameandika shabiki anaetumia
jina la Neyjd.
Chapisha Maoni