MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendeleza mwanzo mzuri katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifungia Cheslea mabao matatu
peke yake katika ushindi wa 4-2 dhidi ya
Swansea City Uwanja wa Stamford Bridge, Londo.
Wakati mchezaji huyo bora wa Agosti, akipiga hat trick yake ya kwanza England na kufikisha
mabao saba ndani ya mechi nne, bao lingine la Chelsea lilifungwa na mchezaji mpya, Loic Remy aliyeingia kuchukua nafasi ya Coasta kipindi cha pili. Beki John Terry alijifunga
kuipatia Swansea ambayo bao lake lingine lilifungwa na Jonjo Shelvey.
Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois,
Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic,
Fabregas/Salah dk82, Schurrle/Ramires dk46, Oscar, Hazard na Diego Costa/Remy dk72.
Swansea: Fabianski, Rangel, Amat/Fernandez dk46, Williams, Taylor, Ki, Shelvey, Sigurdsson, Dyer, Routledge/Montero dk66 na Gomis/Bony dk76.
Chapisha Maoni