KAMATI Kuu ya Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA) imepiga kura kuzuia umiliki wa tatu wa wachezaji ambao umekuwa ukiruhusu wawekezaji wa nje kunufaika na uhamisho.
Rais wa FIFA, Sepp Blatter amesema kikosi kazi kitaandika sheria sasa ya kufuata. Uamuzi huo wa leo ni ushindi wa kisiasa kwa Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) na Rais wake, Michel Platini, ambaye amekuwa akirudia kuitaka FIFA kuchukua hatua.Umiliki wa panda tatu ni maarufu kwa
mawakala, wawekezaji na klabu za Latin
Amerika, Hispania na Ureno, lakini tayari
umezuiwa nchini England.
Licha ya hivyo, klabu kadhaa za Ligi Kuu
England zimeripotiwa kununua wachezaji kwa wamiliki wa tatu pia ili kufanikisha nyota zilizowasajili msimu huu.
Eliquim Mangala aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 32 kutoka Porto kwenda Manchester City, Marcos Rojo Pauni Milioni 16 kutoka Sporting Lisbon kwenda Manchester United na Lazar Markovic Pauni Milioni 20 kutoka
Benfica kwenda Liverpool wote waliripotiwa kununuliwa kwa wamiliki watatu.
UEFA inasema uhamisho wa aina hiyo
unazigharimu klabu fedha nyingi wakati wa kununua wachezaji na wakati mwingine unawakwamisha wachezaji wanapotaka kununuliwa na klabu ambazo haziko tayari kulipa kwa wamiliki watatu- na haina msaada
kwa mchezaji ambaye anaachwa na klabu.
Chapisha Maoni