Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
akihutubia Baraza Kuu la 69 la Umoja wa
Mataifa siku ya Alhamisi ambapo pamoja
na masuala mengine alitoa wito kwa
Jumuiya ya Kimataifa wa kutoinyanyapa
Afrika kwa sababu ya Ebola na kusisitiza
kuwa Afrika ni Bara la lenye nchi 53 na
kwamba si nchi zote zenye Ebola kauli
iliyopigiwa makofi na wajumbe wa Baraza
Kuu la 69 waliokuwa wakimsikiliza ikiwa
ni ishara ya kuunga mkono kauli yake.
Na Mwandishi Maalum,
New York
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete
ameungana na viongozi wengine duniani
katika kuichagiza Jumuiya ya Kimataifa
kuzisaidia Liberia, Siera Leone na Guinea
mataifa ambayo yameathirika vibaya na
mlipuko wa Ugonjwa wa Ebola. Amesema
misaada inayopelewa na itakayopelewa
katika nchi hizo inatakiwa kuwa endelevu
na ya uhakika hadi pale ugonjwa huo
utakapodhibitiwa.
Rais Kikwete ametoa wito huo siku ya
alhamisi wakati alipokuwa akilihutubia
Baraza Kuu la 69 la Umoja wa Mataifa
katika majadiliano ya jumla ( General
Debate) yaliyoanza siku ya jumatano hapa
Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa. Akaongeza pia kwamba nchi za
Afrika ya Magharibi na nyingine barani
Afrika zinatakiwa kujengewa uwezo
ukiwamo wa namna ya kuchunguza
ugonjwa huo, kuwa na maeneo maalum ya
wagonjwa pamoja na huduma za
matibabu. Kwa mujibu wa Rais Jakaya
Kikwete juhudi zaidi zinatakiwa kufanyika
za kufanikisha upatikanaji wa tiba ya
uhakika ya ugonjwa huo, tiba ambayo
amesema itasaidia pia kuimarisha afya za
wale ambao tayari wameathiria.
Akizungumzia zaidi kuhusu mlipuko wa
Ebola na athari zake, Rais ametaka
kuwapo kwa ushirikiano ndani ya jumuiya
ya kimataifa hususani nchi zenye uwezo
mkubwa wa kifedha na utaalam ili kwa
umoja wao waweza kuwasaidia
wanasayasi ambao wanaendelea na
jitihada za kutafuta tiba na chanjo ya
ugonjwa wa Ebola. Pamoja na kutaka
mataifa yaliyoathirika na Ebola kusaidiwa
kwa hali na mali, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzani ameitaka pia
Jumuiya ya Kimataifa kutoinyanyapaa
Afrika kwa sababu ya Ebola.
Akasema taarifa za kuwapo kwa watu
wanaofuta au kuahirisha safari zao za
kwenda Afrika eti kwa sababu ya Ebola
zinasikitisha.“Umoja wa Mataifa na
Marafiki wa Afrika,saidieni kuwaeleza
kwamba Afrika ni Bara lenye nchi
53.Afrika siyo nchi moja, Nchi nyingi ziko
mbali sana na nchi nchi ambazo
zimeathirika kwa Ebola. Na kwa kweli
pengine nchi zilizoathirika ziko karibu
zaidi na Ulaya kuliko mataifa mengine ya
Afrika”.
Akaongeza “Tusaidieni kupaza sauti ya
Afrika ya kutonyanyapaliwa kwa sababu ya
Ebola” akasema Rais. Kauli iliyopigiwa
makofi na wajumbe waliokuwa
wakimsikiliza.
Katika hotuba yake pamoja na
kuuzungumzia kwa kina mlipuko wa
Ebola, Rais Kikwete pia alizungumzia
kuhusu maeneo mengine muhimu hususani
katika Usalama wa Kimataifa, ambapo
aligusia matukio ya kigaidi
yanayoendeshwa na makundi kama Al
Shaabab, ISIS na Boko Haram katika
maeneo mbalimbali na kwamba makundi
hayo hayapashwa kuachwa kuendelea na
uovu wao.
Akayataja maeneo mengine ambayo
yanaendelea kuifanya dunia kutokuwa
mahali salama kuwa ni pamoja na
mwendelezo wa uvunaji haramu wa mali
asili, uwindaji haramu, biashara haramu
ya dawa za kulevya na silaha. Aidha
ametoa wito wa kutafutiwa ufumbuzi wa
kudumu wa migogoro inayoendelea huko
Libya, Jamhuri ya Afrika ya Kati na
Sudani ya Kusini. Kuhusu Palestina Rais
amesema dunia haihitaji kusubiri zaidi
hasa kutoka na mikasa ambayo
imesababisha maisha ya watu wasiokuwa
na hatia wakiwamo watoto, wanawake na
wanaume kupotea bila sababu.
Na kwa sababu hiyo ametoa wito wa Umoja
wa Mataifa, Marekani, Urusi na Mataifa
ya mengine ya Ulaya yafikie mahali pa
kuutafutia ufumbuzi wa kudumu mgogoro
kati ya Palestine na Israel jambo alilosema
kuwa linawezeka.
Kwa upande wa Sahara ya Magharibi
ambalo ni koloni pekee barani Afrika, Rais
Kikwete ameiutaka Umoja wa Mataifa na
wadau wengine kulitafutia ufumbuzi ili
nalo lifike tamati.Rais pia alizungumza
tatizo la muda mrefu la vikwzo vya
kiuchumi ambavyo imewekewa Cuba,
akazungumzia pia tatizo na changamoto
ya mabadiliko ya Tabia nchi,na mchakato
wa maandalizi ya malengo mapya ya
maendeleo endelevu ambayo alisema
Tanzania iko tayari kushirikiana na
mataifa mengine katika eneo hilo.
Chapisha Maoni