0
HOJA ya kusitisha Bunge Maalum la Katiba imehitimishwa rasmi Kisheria kwa Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutamka kwamba bunge hilo
linaweza kuendelea na shughuli zake.
Taarifa hiyo imetolewa jana 15 Septemba, 2014 na Mjumbe wa Kamati namba Tano, Mhe. Dkt. Asha-Rose-Migiro wakati wa mjadala wa jioni bungeni hapo.

Akisoma taarifa hiyo, Dkt. Migiro amesema kuwa mjadala wa kusitisha bunge umefungwa rasmi hapo jana licha ya kuwepo kwa madai kuwa bunge hilo halina uhalali wa kisiasa.

“Kwaajili ya kuondoa shaka yoyote
ningependa kuwaambieni takwimu
tulizonazo hivi sasa, bunge hili lina jumla
ya Wajumbe 630, kati ya hao waliotoka ni
wajumbe 130 ambao ni sawa na asilimia
21% tu ya wajumbe wote, wajumbe
waliobaki ndani ya bunge ni 500 hii ni
sawa na asilimia 79% ya wajumbe wote na
tukizichambua takwimu hizi, ningeomba
kutambua wingi wa Kundi la 201”, alisema Dkt. Migiro.

Akikanusha juu ya kuwepo kwa dhana
iliyojitokeza ya kwamba wajumbe waliobaki ndani ya bunge hilo ni wa aina moja, Dkt. Migiro alisema kuwa taarifa hizo si za kweli, kwani kati ya wajumbe 500 walioko ndani ya bunge hilo wajumbe wanaotokana
na kundi la 201 ni wajumbe 189 ambapo
wajumbe wanaotoka Tanzania bara jumla yao ni 348 na kati ya hao, 125 ni wajumbe wanaotoka katika kundi hilo la 201.

“Ukitazama takwimu hizi kwa jicho lolote
lile basi wajumbe wa 201 ni sehemu kubwa na ni sehemu muhimu ya wajumbe hawa waliobaki”, alisema Dkt. Migiro. Akizungumzia juu ya wajumbe toka upande wa Zanzibar, Dkt. Migiro alisema kuwa wajumbe waliobaki ni 152 na kati ya hao wajumbe 64 wanatokana na kundi la 201.

“Tunasisitiza takwimu hizi kwa wajumbe
wa 201 kwasababu wajumbe hawa ndiyo wajumbe ambao kwa wingi wao kitakwimu lakini pia kwa wingi wao kimakundi wanawakilisha sura zote Kitaifa, hivyo ni dhairi kwamba kwa namna yoyote ile
waliobaki ndani ni wengi, ni idadi kubwa,
ni idadi wakilishi na tukiangalia kwa
takwimu hizi, wajumbe walioamua kususia bunge kwa pande zote mbili hizi hawafikii hata theluthi moja ya wajumbe waliobaki”, alisisitiza Dkt. Migiro.

Kwa kuzingatia matakwa ya kisheria, Dkt. Migiro alieleza kwamba uamuzi upatikane
kwa maridhiano, kwa majadiliano na kwa kushawishiana kwa hoja wajumbe
waliobaki na walio wengi wanaweza
wakatumia wingi wao na wana uhalali wa
kisiasa na wa kisheria.
Dkt. Migiro aliendelea kusema kuwa,
wajumbe waliotoka hawakuona kuwa
utaratibu huo ungekuwa na manufaa kwao
licha ya kuwepo na maridhiano katika
bunge hilo, pia kupitia wadau mbalimbali
Vyama vya siasa vyote vimekuwa
vinazungumza nje ya bunge kupitia Msajili wa Vyama vya siasa, kupitia Kituo cha Demokrasia (TCD) na kupitia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Chapisha Maoni

 
Top