Kama wewe ni mmoja kati ya ‘waliodata’
na ngoma ya Linah aliyofanya Afrika
Kusini akiwashirikisha Uhuru, tegemea
kudata zaidi na ujio mpya wa msanii
chini ya kampuni ya kimataifa ya ‘No
Fake Zone’ , ameiambia tovuti ya Times
Fm kuwa wimbo unaofuata utakuwa
mkubwa zaidi ya Ole Themba na
kwamba amefanya na msanii mkubwa
sana Afrika.
“Yaani inakuja kubwa zaidi ambayo hiyo
itakuwa funika, waswahili wanasema
itakuwa ‘ndio basi tena..’ (anacheka).
Nimeshaifanya ila kuna baadhi ya vitu
ambavyo naenda kumalizia. Kwa hiyo
Mungu akijalia hizo wiki zinazokuja
ntaenda (Afrika Kusini) kumalizia.” Linah
ameiambia tovuti ya Times Fm.
Hata hivyo hakumtaja msanii huyo
aliyefanya nae kazi na kuahidi kuwa
itakuwa surprise baada ya kazi
kumalizika na kutoka kama ilivyokuwa
‘Ole Themba’ .
Katika hatua nyingine, Linah ameeleza
kuwa wimbo wake Ole Themba umempa
mafanikio makubwa ambayo hakuwahi
kuyafikia na kwamba sio Tanzania tu bali
Afrika kwa ujumla kwa kuwa video yake
imechezwa katika vituo vingi sana
vikubwa.
Usikose kusikiliza Bongo Dot Home ya
100.5 Times Fm Jumamosi hii kuanzia
saa 10 kamili jioni utamsikia Linah
akieleza mengi ikiwa ni pamoja na
ufafanuzi baada ya kuchaguliwa kuwa
balozi wa wanawake na Uchumi.

Chapisha Maoni