0
Jeshi la polisi mkoani Mtwara limefanikiwa
kudhibiti maandamano ya chama cha
maendeleo na demokrasia Chadema kwa
kufanya doria kila kona ya mji huo huku
wakiwa wamejiandaa kwa vifaa ili
kupambana na yeyote atakayejaribu kuvunja katazo la jeshi hilo la kuzuia maandamano mkoani humo.

Hata hivyo ITV imeshuhudia jeshi hilo likiwa katika gari la polisi likipita maeneo
mbalimbali likiwemo eneo la Mkanaledi
ambalo lilitajwa maandamao ya Chadema yataanzia huko na hatimaye kuingia katikati ya mji.

Akizungumzia ulinzi huo kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Augustino Ulomi amesema wamelazimika kutawanya askari kila kona sambamba na kuwaita viongozi wa chama hicho kuwahoji baada ya kugoma kutii amri
ya jeshi hilo ya kuzuia maandamano na
kuamua kusambaza vipeperushi vya
kushawishi wananchi kujitokeza katika
maandamano kupinga kuendelea kwa bunge maalum la katiba Kwa upande wake mwenyekiti wa chadema
wilaya ya Mtwara Ibrahimu mandoa
amesema pamoja na jeshi la polisi
kufanikiwa kudhibiti maandamano hayo zipo njia mbadala za kufikisha ujumbe kwa umma na serikali.

Kwa upande wa wananchi wameonekana kutounga mkono maandamano hayo kwa madai waadhirika wakubwa ni wao.

Chapisha Maoni

 
Top