kwamba, mapenzi yanachukuwa sehemu
kubwa sana ya maisha yetu ya kila
siku.Tunafanya kazi usiku na mchana
lakini pesa tunazopata tunazitumia
kwenye kufurahia maisha na wapenzi
wetu.Ndiyo maana ukiwa hauko sawa
kimapenzi, namaanisha ukiwa huna
mpenzi wakati unahitaji kuwa naye au
unaye lakini anakukorofisha, hata
mambo mengine huwezi kuyafanya kwa
ufasaha.
Lakini yule ambaye maisha yake ya
kimapenzi yako sawa, anapata
anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake,
utagundua anafanya kazi kwa ufanisi
mkubwa na furaha haikauki.Wakati
ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao
wanaachika kila siku kwa sababu ya
kushindwa kujua namna ya kuwashika
wapenzi wao. Kuna ambao kusalitiwa
kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa
sababu hawajui yapi wayafanye ili
wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya
uhusiano wao.
Kimsingi nimegundua wengi hatuna
elimu ya kutosha juu ya mapenzi.
Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu
ambaye yuko mbali lakini hajui
wanawezaje kulidumisha penzi lao.
Mmeoana wote mnafanya kazi na ni
wanandoa, mnawezaje kuishi katika
msingi sahihi? Hayo yote utayajua
endapo tu utajua sehemu sahihi ya
kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu
kuhusu mambo hayo.
Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi
kujihusisha kimapenzi, leo umeingia
kwenye uhusiano na hujui chochote,
kama huna elimu ya mapenzi hata kama
umzuri vipi, utaachika tu kama siyo
kusalitiwa kila siku.
Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili
kama ulikuwa hujui, uanze leo
kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba.
Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi ya
kiutu uzima, yale ambayo huwezi
kufundishwa shuleni, kusoma kwenye
magazeti, kuona kwenye vipindi vya
kawaida vya televisheni au kusikisiliza
redioni. Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana
katika ulimwengu wa sasa. Hakuna
ambalo utalihitaji usilipate kwenye
mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama
kuna jambo unataka kulijua kuhusu
mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao
husika.
Kwa mfano unataka kujua jinsi
unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako
mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao,
utakuletea.Licha ya kwamba lugha
unayotumika ni ya Kiingereza, naamini
wengi wetu tunajua hata kama ni cha
kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada
ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza
kuzipata.
Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia
mapenzi kwa undani wake ambayo
yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya
watu wazima tu. Kama kweli wewe ni
mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo,
ukiulizia utayapata kwani huwezi
kuyakuta yanauzwa kiholela.
Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa
lakini elimu utakayoipata ni kubwa na
huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa
mfano unanunua jarida la shilingi 50,000
na ndani yake ukapata mada juu ya
kuishi kwa furaha na mpenzi wako,
namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya
kumpagawisha mpenzi wako muwapo
faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni
pesa ndogo ukilinganisha na gharama
ulizotumia kwenye harusi yenu?
Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya mapenzi
ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano
mimi nimekuwa nikitumia muda wangu
mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya
mambo yanayowakosesha furaha katika
maisha yao ya kimapenzi.
Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo
baadhi ya akina mama ambao
wamekuwa wakitumika sana kwenye
kuwafunda wasichana kabla ya kuingia
kwenye ndoa.Kikubwa ni kujua watu
sahihi wa kuwauliza mambo sahihi
kuhusiana na mapenzi. Nilichogundua
mimi ni baadhi ya watu kuwa na aibu.
Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua
mambo nyeti ambayo unajua
kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha
ndoa yako?
Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu na elimu hasa hii
nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali
kuamka usiku na kuangalia vipindi
ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa
watu wazima.Mara nyingi vipindi hivi
huwezi kuviona mchana, wanaovirusha
husubiri muda ambao watoto wamelala.
Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi
hivi, ni lazima utakuwa bora kwenye
uhusiano wako.
Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza
zaidi kupitia mimi, usisite kunitafuta.
Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo
vinaweza kudumisha ndoa yako lakini
ukiwa unaendesha maisha yako
kibubusa, kaa mkao wa kusalitiwa kama
siyo kuachwa!
Chapisha Maoni