MADAMUUU! Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ amecharuka na kudai anachukizwa kwa kiasi kikubwa na wasanii ambao wanapenda kumfanyia majungu kutokana na chuki
zao binafsi.
Akipiga stori na paparazi wetu, Madam alisema anajua wapo wengi wanaomchukia kutokana na sababu zisizo za msingi kwa kudai kuwa anaringa na vyovyote vile wanavyojadili lakini hajali kwa kuwa hakuna ukweli wowote.
“Watu wenye majungu hawanisumbui kichwa kabisa nabaki nawatazama tu, sababu sina maringo wala majivuno kwa mtu yeyote, sasa cha ajabu wengine wanasema naringa, kwa staili hiyo
hatutafika mbali maana wasanii wa nchi za wenzetu wana umoja hawana mambo ya aina hiyo,” alisema Wema.
Chapisha Maoni