linalowakabili baadhi ya watu katika
jamii, wengi wakiwa wanaume. Tatizo
hili linaonekana kuzidi kuwa sugu, hali
inayosababisha kuwepo na harufu
mbaya hasa kwenye mikusanyiko na
wengi wao huwa wagumu kukubaliana
na hali yao hata kutafuta tiba mahususi
inaweza kuwaondolea kero hiyo.
Licha ya kuwepo sababu mbalimbali
zinazochangia kutokea hali hiyo, ukweli
utabaki kuwa uchafu ndio chanzo kikuu
cha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta
harufu mbaya kwenye miguu na
kuwakera wanaokumbana na harufu
hiyon.
TIBA YAKE.
Pamoja na tiba nyingine za kitaalamu
ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza
kupata, usafi ni jambo kubwa
analopaswa kuzingatia zaidi. Ukigundua
una tatizo hili, hakikisha unasafisha
miguu, viatu na soksi zako mara kwa
mara ili kuepusha unyevunyevu.Epuka
kurudia soksi au kuvaa ambazo
hazijakauka vyema kwani zinaweza
kusababisha miguu kunuka mara
dufu.Usivae viatu vilivyoloa na endapo
ikatokea umenyeshewa, hakikisha
unavianika kwenye hewa ili vikauke
kupunguza uwezekano wa kutokea
harufu.
Kama utahisi tatizo ni kubwa zaidi ni
vyema utumie sabuni au poda zenye
dawa za kuua vijidudu pamoja na
mafuta maalumu yanayoweza kutumika
miguuni. Unaweza kusugua miguu kwa
kutumia chumvi, chokaa au kuvaa open
shoes na sendo kuepuka tatizo
ili.Ikishindikana, nenda kwa wataalamu
wa afya.
Chapisha Maoni