0
Habari mpya zinasema kuwa vikao vya
harusi ya Diamond na Meninah ambaye
ni mwanamuziki wa Bongo fleva
vimeanza kimya kimya nyumbani kwa
mama Diamond huku mmoja wa
wahudhuriaji wakiwa ni mama Diamond
mwenyewe na Queen Darling ambaye ni
dada wa Diamond.
Kwa mujibu wa Baabkubwa magazine
paparazzi wake alienda nyumbani kwa
Diamond hivi juzi kati kufanya nae
mahojiano hata hivyo hakumkuta
Diamond lakini alimkuta mmoja wa
watu wake wa karibu ambaye yupo pia
upande wa Wema Sepetu.
Chanzo hicho kilimwaga news kuwa
hakuna cha ndoa ya Diamond na Wema
bali ndoa inayopangwa kwasasa ni ya
Diamond na Meninah na vikao vimeanza
kwa mama Diamond. Chanzo hicho
kilisema kuwa Diamond na Meninah
walikutana takribani miezi mitano
iliyopita wakati wa maandalizi ya tuzo za
Kili Awards 2014 ambapo wote
walitumbuiza. Baada ya hapo wakaingia
mapenzini kimya kimya mpaka wiki za
hivi karibuni gazeti moja lilipovujisha
habari hizo za mahaba ya Diamond na
Meninah na media nyinmgine
kuziandika kwa kasi.

Kwa mujibu wa chanzo hicho ni kuwa
Wema ametoswa sababu ya kuendekeza
pombe inayompelekea kuwa mvivu na
kutotaka kufanya kazi badala yake ni
starehe tupu, kwa maana kuwa hata
nyumbani kwa mama Diamond haendi
mara kwa mara kumsalimia inaweza
hata kupita miezi 3 hajaenda ila Meninah
anaenda na akifika kule humsaidia
mama Diamond kazi, kupika na
kupakua. Chanzo hicho kimesema kuwa
hata Wema anajua kuwa Diamond na
Meninah wana ishara zote za kuwa
wapenzi lakini hana cha kufanya, huku
Meninah yeye akiwa tayari amejitoa
muhanga kwa Diamond lakini
anawaogopa Team Wema kumshambulia
hasa kwa mvua za matusi kama ilivyo
kawaida yao lakini mama Diamond
anampoza kuwa asiwe na shaka yeye
kamkubali Diamond hawezi kukataa
kumuoa hilo amuachie yeye mama
Diamond.
Vikao hivyo licha ya kuhudhuriwa na
mama Diamond na Queen Darleen,
chanzo hicho kimesema pia kuwa kuna
ndugu wengine wa Diamond na mama
Diamond wanahudhuria ila yeye hawajui
sababu hana ukaribu nao.

Chapisha Maoni

 
Top